Picha za Buhari za hivi punde akiwa London zachapishwa

Haki miliki ya picha Muhammadu Buhari/twitter
Image caption Picha za Buhari za hivi punde akiwa London zachapishwa

Ujumbe wa hivi punde kwenye mtandao wa twitter kutoka kwa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mjini London, ambapo alienda kwa likizo ya matibau, unaonyesha picha akikutana na kasisi mkuu wa Canterbury.

Makamu wa Rais Yemi Osinbajo kwa sasa ndiye kaimu rais nchini Nigeria huku Buhari akiwa London.

Buhari hajarejea nchini Nigeria kwa wiki ya saba sasa na kuzua wasi wasi nchini humo, huku watu wakijiuliza maswali mengi kuhusu kile kilichomkumba Rais.

Sababu ya Buhari kuchukua likizo ya kimatibabu bado haijatajwa.