Ziwa la rangi ya waridi nchini Australia

Ziwa la maji ya rangi ya waridi Australia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ziwa la maji ya rangi ya waridi Australia

Ziwa moja la maji ya chumvi mjini Melbourne Australia limegeuka na kuwa na rangi ya waridi kutokana na mwanga wa jua, joto na mvua chache.

Maafisa wa mbuga za wanyama pori wamesema kuwa mwani unaomea katika ziwa hilo chini ya bustani ya Westgate hutoa rangi nyekundu.

Furahia mandhari lakini nawashauri kutoshika maji hayo,alisema victoria.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ziwa la rangi ya waridi

Hali hiyo pia hutokea katika eneo la salina Torrevieja katika ziwa la Dusty Rose na ziwa la Retba nchini Senegal.

Mwanasayansi wa maswala ya kuhifadhi katika bustani ya Victoria amesema kuwa rangi hiyo imesababishwa na mwani kwa jina Dunalliela.

''Sisi hupata maoni kwamba bustani hiyo huonekana kana kwamba ni kiwanda cha rangi kilichomwaga rangi hiyo kwa bahati mbaya''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bustani ya victoria nchini Australia

Dkt Norman amesema kuwa ijapokuwa maji hayo sio hatari ,hangemruhusu mtu kuogelea.

Wasimamizi wa ziwa hilo wamesema kuwa wanataraji kwamba ziwa hilo litabadilika na kuwa yangu yake ya kawaida wakati joto litakapokwisha na mvua kuongezeka.