Mabaraza yachangamkia uchoraji wa mitaani Uingereza
Huwezi kusikiliza tena

Mabaraza yachangamkia uchoraji wa mitaani Uingereza

Sanaa ya uchoraji mitaani imeanza kuchangamkiwa na manispaa pamoja na mabaraza miji nchini kote Uingereza kuleta mrashio wa rangi na kizazi kipya mitaani na mijini.

Mwezi Januari manispaa ya Croydon jijini London ni karibuni tu kutangaza kuwa maeneo mengi ya umma mitaani sasa yanaweza kuchorwa kwa rangi za kupuliza.

Lakini kwa baadhi yao hatua hiyo haina tofauti na uchorati wa kupuliza usioruhusiwa ambao halmashauri zinatumia mamilioni ya pauni kila mwaka kuifuta. Zawadi Machibya anaarifu zaidi.