Donald Tusk azua mgawanyiko Poland

Tusk
Maelezo ya picha,

Donald Tusk

Mgawanyiko mpya umetokea ndani ya Umoja wa Ulaya kuhusu kuchaguliwa tena kwa Donald Tusk kuwa Rais wa baraza la Mawaziri la Ulaya.

Kukataliwa kwa Tusk na Poland nchi alikotoka hakujaungwa mkono na nchi wanachama wa Umoja huo, ambao wametupilia mbali ombi la Warsaw la kucheleweshwa kwa kura

Waziri mkuu wa Poland Beata Szydlo amewaambia waandishi wa habari kuwa itakuwa makosa kumchagua tena Tusk kinyume na ombi la Poland, anasema hakuna makubaliano ndani ya umoja huo kuwa rais anaweza kuchaguliwa bila nchi anayotoka kuridhia.

kwa sasa Malta inashikilia kiti cha urais ndani ya EU. Akiwasili kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, waziri mkuu wa Malta, Joseph Muscat , ameeleza kuwa Poland peke yake haitaweza kuzuia kuchaguliwa tena kwa Donald Tusk

'' Nchi moja , au nchi kadhaa zinaweza kutounga mkono maamuzi lakini nchi moja haiwezi kuzuia uamuzi wa chombo hiki, kwa sababu kuna taratibu za wazi kabisa za kufuatwa, hivyo sheria na taratibu zitafuatwa''

Maelezo ya picha,

wajumbe wa baraza la mawaziri

Naye waziri wa mambo ya nje wa Poland Witold Waszczykowski amesema nchi yake itafanya kila iwezalo kuzuia kura kwenda kwa Tusk, Chama tawala Pis cha Poland kinampinga bwana Tusk ambaye alikuwa Waziri mkuu wa zamani kutoka chama pinzani.

Akiongea kwa nji ya Televisheni kiongozi wa bunge la seneti nchini Poland Stanislaw Karczewski amesema mgombea mwingine yeyote atakubalika isipokuwa Tusk

''Tunajua kilichotokea miezi kadhaa iliyopita, tunajua namna Donald Tusk alivyoshughulikia suala la siasa za Poland, alionekana akiunga mkono upinzani bila sababu, aliwakilisha upinzani, alifanya vibaya sana. Kama kiongozi wa baraza la Umoja wa Ulaya hakupaswa kufanya hivyo, hakutakiwa kuegemea upande mmoja, ninashawishika kuwa mwanasiasa yeyote asingekubaliana na matendo yake''