Trump apingwa tena juu ya sheria ya uhamiaji

Image caption Wahamiaji kutoka nchi ya kiislamu,wakiwa uwanja wa ndege ,New York

Kumekuwa na changamoto zaidi za kisheria dhidi ya marufuku ya Rais Donald Trump kuhusu wahamiaji kutoka nchi sita za Waislam.

Siku moja baada ya Jimbo la Hawaii kufungua kesi, Jimbo la Washington nalo linafungua kesi likiungwa mkono na New York, Massachusetts na Oregon.

Washington waliongoza mapambano dhidi ya tamko la kwanza la Rais Trump na walishinda baada ya Jaji wa mahakama kuu kukubaliana na zuio la hatua hiyo kwa nchi nzima.

Sasa mwanasheria wa jimbo hilo, Bob Ferguson amemuomba Jaji kuendeleza msimamo huo hata kwa hatua ya pili ya Rais kwa kuwa bado inakiuka Katiba.