UN haitafunika uovu wa vikosi vya walinda amani

Haki miliki ya picha Google
Image caption Antonio Gutteres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres ametoa mapendekezo kadhaa yenye lengo la kupambana na unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kwa wakazi wa maeneo wanakofanya kazi.

Bwana Guterres anasema malipo kwa ajili ya nchi ambazo hupeleka askari wa kulinda amani zishikiliwe iwapo uchunguzi hautafanyika kwa ufanisi.

Chini ya sheria ya Umoja wa Mataifa, nchi zinazochangia walinda Amani zinawajibika kuwawajibisha askari wake.

Bwana Guterres anasema fedha hiyo inaweza kwenda katika mfuko wa waathirika; amependekeza pia kuteua mawakili maalum kusaidia walioathirika.

Aliongeza kwa kusema kuwa bendera ya Umoja wa Mataifa haitatumika tena kufunika uovu unaofanywa na vikosi vya walinda usalama