Wanajeshi wa US wasambaza picha za utupu za wenzao wa kike

Wanajeshi wanawake Haki miliki ya picha Huw Evans picture agency
Image caption Wanajeshi wanawake wa Marine

Wanajeshi wa Marekani kutoka vitengo tofauti vya jeshi wamekuwa wakionyeshana picha za uchi za wanajeshi wenzao wa kike kwenye mitandao.

Ripoti ya wiki iliyopita ilibaini picha nyingi za uchi zilizokuwa zikisambazwa na kitengo cha wanajeshi wanamaji wa zamani na wanahudumu kwa sasa katika mtandao wa Facebook kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Lakini BBC imeona picha ambazo wanajeshi wengine kutoka vitengo vyengine ambao wamesambaza mamia ya picha hizo.

Makao makuu ya kijeshi ya Marekani, The Pentagon, yamesema tabia hiyo 'haiambatani' na mila zake.

Wanajeshi wanaume wamekuwa wakitumia mtandao wa picha na video wa Anon -IB kuweka picha hizo za uchi za wanajeshi wenzao wa kike.

Wanajeshi hao kwanza huweka picha za wanawake hao wakiwa na nguo ambazo huzitoa katika kurasa za mitandao yao ya kijamii, na kuuliza wengine katika kundi hilo iwapo mmoja wao anapicha za uchi za mwanajeshi huyo, ambao huita 'ushindi' na wengine hutuma picha hizo za uchi.

Chapisho hizo wakati mwengine huambatana na majina na hata kitengo wanachohudumu kuhusiana na mwanajehi hao wa kike.

Kundi la Facebook la Marines United linalowajumuisha wanachama 30,000 lilifungwa hivi majuzi baada ya kisa hicho kujulikana.

Kamanda mkuu wa wanamaji hao amekitaja kisa hicho kama cha''aibu.''

Nikisikia madai ya wanamaji wakiwadumaza wenzao , sidhani tabia kama hizo ni za ''wapinganaji wa kivita walio stawi,'' Gen Robert Neller alisema mapema wiki hii.

Watumizi wa mtandao huo hutuma picha zilizopigwa na wanawake wenyewe wakiwa na nguo za kuogelea za bikini na bila nguo za juu.

Idara ya ulinzi ya Marekani imesema katika taarifa yake ilikuwa imetoa ''muongozo wa sera,'' ili kujikinga na kukabilianana visa vya ''unyanyasaji wa kijinsia. ''

Ukurasa wa Facebook wa Marines United umefungwa.