Mama anayemnunulia heroine mwanawe

Picha ya katuni
Image caption Picha

Utafanya nini iwapo mtoto wako ana uraibu wa Heroin na sasa anaugua dalili za baada ya kutumia dawa za kulevya .

Akisubiri kupata matibabu kutoka kwa kituo cha kurekebishia tabia, mwanamke kutoka kijiji kusini magharibi mwa Uingerea alieleza jinsi alivyompeleka mtoto wake mjini na kumlipia hela apate matibabu.

Mtoto huyo alikuwa anatokwa na jasho, atapika , analia na kutetemeka akijihisi kuwa mgonjwa.

''Nilijihisi ni kama nimeingia mtegoni na sikuwa na la kufanya'' . Hapo nikamuuliza , ''kuna jambo lolote tunaweza fanya kwa hivi sasa ?''

Mama huyo alitumia zaidi ya saa moja unusu akiwapigia watu tofauti na watu wote walimsihi atumie Heroin na sio dawa inayopunguza dalili za baada ya kutumia dawa za kulevya methadone .

Hivyo ndivyo tulivyosalia katikati mwa mji na nikanunua dawa hiyo.

Shida hiyo ilianza miaka mitano iliyopita alipokuwa na umri wa miaka 18 . Alianza kupata marafiki wapya alipokuwa akienda chuo kikuu na maisha yake yakaanza kubadilika kabisa kitabia na mienendo yake.

Image caption Picha

Hapo awali alikuwa mwenye bidii ,alimpenda farasi wake na angempeleka lakini mambo yalianza kubadilika polepole . Alipenda kulala sana mchana , na nilikuwa nikimuuliza alikuwa na shida gani?

Baadaye alianza kutembea na watu ambao tuliwafahamu hawakuwa na maadili mema na watu waliomzidi umri na waliokuwa wakitumia madawa. Hapo mambo ndipo yalipoanzia.

Tulikuwa tumetoka safari siku moja na nikamuuliza tena nini humsumbua ?

Na akajibu ,''fikiria kitu kibaya na itakuwa hicho''

Mama akamuuliza , ''Unamimba?'' ,nikiifikiria sasa haingekuwa kitu. Ingekuwa kitu kizuri kwa upande mwengine , iwapo hilo lingekuwa jawabu, kwa sababu jibu lilikuwa: hapana, hapana mama. Fikiria kitu kibaya zaidi , kibaya zaidi ya hicho ?'' akamuuliza

Mamake akamuuliza , una uraibu wa dawa za kulevya?'' na akasema ''Ndio''

Akaanza kulia , ilimvunja moyo. Ilikuwa siku yangu mbaya maishani.