Mwanariadha anayezimia mara 15 kwa siku

Katie Cookie

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19 kutoka Cherrywood , kusini mwa Dublin , anaugua kile daktari wake amekitaja kama ''kifafa'' na huzimia zaidi ya mara 15 kwa siku na kupoteza fahamu.

''Mwili wote hutetemeka ,misuli kutoka, na mtu hujihisi kila kitu kimetolewa kutoka kwa mwili wake na hauwezi kuvuta pumzi , alisema.

''Kila siku sina udhibiti.''

Licha ya kukumbana na kupoteza fahamu mara kadhaa anapokimbia , Cooke alishinda tuzo za mbio za mji wa Dublin za kilomita 5.

Alikimbia mbio hizo kwa dakika 17. Amekuwa akionekana mtaani na mwenzake ambaye ni daktari Colin Doherty wakikimbia , daktari wake wa maswala ya ubongo.

Lakini si mwanariadha wa kila wakati.

Alipatikana na ugonjwa huo akiwa na umri wa miaka 9 , alianza kutumia madawa hadi pale ugonjwa huo ulipozidi alipoanza kubalehe , ambapo homoni zake zilianza ''kuchangamka. ''

''Sikuwa na uwezo wa kutoka kitandani, sikuwa naweza kujifanyia kitu chochote binafsi na singeweza kuzungumza. Mamangu aliniosha na kunivalisha nguo,''alisema Cooke

Cooke alilazwa katika hospitali ya Our Lady Children mjini Crumlin kwa miezi kumi licha ya kufanyiwa majaribio ya dawa tofauti , bado alipata dalili hizo hizo, hangeweza kudhibiti mgongo wake na sehemu ya nyonga na wakati alipotolewa hospitalini hakuwa na uwezo wa kutembea.

''Singeweza kusimama, nilitumia kiti cha magurudumu cha walemavu kwa karibu miezi saba kwa kuwa nilikuwa mtu msumbufu nilitaka kuwaonyesha watu kwamba ningeweza kutembea''.

''Baada ya matibabu ya mazoezi ya mwili , nilianza kukimbia polepole na nikaanza kupenda uhuru wangu niliokuwa nikiutaka.''

Cooke kwa hivi sasa hukimbia kila siku na anasema akikosa mazoezi hayo hujihisi na uchovu mwingi na hupata kisunzi alichokuwa akishuhudia miaka iliyopita.

Lakini kukimbia kunachangia dalili za ugonjwa wake na sio tiba

Ongezeko la mdundo wa moyo unaosababishwa na kukimbia husababisha kupoteza fahamu zaidi ikilinganishwa na iwapo hajakimbia, lakini Cooke amesema anaimarisha maisha yake, si jambo la kukubali kirahisi.

Daktari wake wa akili Dkt Doherty amekuwa akipima faida na hasara kutokana na matibabu anayoyapokea.

Kuna changamoto ya kuugua maradhi ya kifafa na ukimbiaji wa masafa marefu lakini pia mtu ambaye hutembea hukumbana na changamoto hizo pia na lakini faida zake zimepita mathara yake, alisema.

Alisema, mimi ni daktari wa maswala ya kifafa lakini jukumu langu pekee ninapo kimbia na Katie ni kuwakinga watu kumweka kwenye gari ya wagonjwa . Mimi husimama hapo na kusema Katie yuko salama ,niko hapa daktari wake , atakuwa sawa.''

Licha ya Cooke kuzimia mara kadhaa, mwili wake hauhitaji wakati wa kupona , anauwezo wa kusimama tena na kukimbia tena.

Dkt Doherty anadhani mazoezi anayoyafanya yanamsaidia kupona

Katie ni mwanariadha anayezingatia mazoezi, hujifunza vizuri. Nina uhakika ni uzoefu bora kwake, alisema

Kisporti na kimasomo ,Cooke ana uwezo wa kuchanganya maisha yake na uhusiano na mpenzi wake Jack.

Cooke amesema,''mpenzi wangu Jack ni mtu mtulivu sijawahi kuona , hulala licha ya kuzimia kwangu ulio wa kutisha. Huamka wakati usio wa kawaida na nishawahi kumpiga kofi wakati mwengine lakini alipata usingizi.''

Cooke amesema kujamiana hakusababishi kuzimia , lakini wakati mwengine hutokea na wanawake wengi huripotiwa na visa vya kuzimia wakati wa hedhi.