Waliokamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa waachiliwa

Waliakamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa waachiliwa Haki miliki ya picha CULVERWELL FAMIL
Image caption Waliakamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa waachiliwa

Mashtaka yote dhidi ya mwanamume raia wa Afrika Kusini na mpenzi wake raia wa Ukrain, yanayohusu kufanya mapenzi nje ya ndoa katika Milki ya Nchi za Kiarabu yamefutwa.

Emlyn Culverwell‚ 29, na Iryna Nohai, 27, wanaripotiwa kukamatwa baada ya daktari kugundua kuwa Bi Nohai, ambaye alikuwa amehisi maumivu ya tumbo alikuwa mja mzito

Walikamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa kitendo ambacho ni kinyume na sheria katika milki ya nchi za kiarabu.

Mama yake Culverwell, alikuwa ameomba waachiliwe akisema kuwa kosa tu walilolifanya ni kupendana.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Afrika Kusini, haikuwa imefanikiwa kusaidia wawili hao, kwa kuwa hilo lilikuwa ni suala la kifamilia, kwa mujibu wa kituo cha News24.