Japan yaondoa wanajeshi wake Sudan Kusini

Japan yaondoa wanajeshi wake Sudan Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Japan yaondoa wanajeshi wake Sudan Kusini

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ametanza kuwa serikali ya Japan itaondoa wanajeshi wake kwenye kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei.

"Huku Sudan Kusini ikiingia kipindi kipya cha ujenzi wa taifa, tumeamu kusitisha jitihada za ujenzi ambao jeshi letu lilikuwa likitekeleza mjini Juba," bwana Abe alinukuliwa na shirika la hari la Kyodo.

Katibu wa mawaziri Yoshihide Suga, baadaye alisisitiza kuwa kuondolewa huku hakutokani na sababu ya kuzorota kwa usalama maeneo wanajeshi hao walikuwa wakifanya kazi.

Wanajeshi hao wa Japan waliowasili nchini Sudan Kusini mwezi Novemba mwaka 2016, ndio wa kwanza katika kipindi cha karibu miaka 70 kutumwa nje ya nchi, wakiwa na agizo la kutumia nguvu ikiwa itahitajika.

Sudan kusini iliyojitenga kutoka Sudan mwaka 2011, imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013.