Sera ya familia kuwa na watoto 2 yaleta mabadiliko China

Mpango wa familia kuwa na watoto wawili China
Image caption Mpango wa familia kuwa na watoto wawili China

Uchina inasema uamuzi wake wa kuruhusu familia kuwa na watoto wawili badala ya mmoja tu, umeleta mabadiliko thabiti.

Afisa wa upangaji uzazi , amesema watoto milioni 18 zaidi walizaliwa mwaka jana ikiwa ni milioni mbili zaidi kushinda miaka iliyopita.

Lakini mabadiliko hayo ya sera hiyo , hayatazuwia wananchi wa Uchina kwa jumla, kuwa wazee swala ambalo litasababisha wazee zaidi na raia wachache walipa kodi kuweza kuwasaidia hao wazee.

Pia watoto zaidi waliozaliwa siyo wengi kama wakuu walivyotaraji walipobadilisha sera hiyo mwaka wa 2015