Shule mashakani kwa kuchora mnada wa watumwa Marekani

soko la mnada wa watumwa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption soko la mnada wa watumwa

Shule moja katika jimbo la New Jersy nchini Marekani iko mashakani kwa kutoa kazi iliowataka wanafunzi walio kati ya umri wa miaka 10-11 kuchora mabango yanayaoonesha mnada wa watumwa.

Baadhi ya wazazi walikasirishwa na hatua hiyo walipoona mabango hayo yamewekwa ukutani.

Mkuu wa shule hiyo aliomba msamaha kwa uchungu uliosababishwa.

Maafisa wa wilaya hiyo walisema kuwa wanafunzi walitakiwa kujua kuhusu baadhi ya nyakati zilizokuwa mbaya katika historia lakini wakakubali kwamba mabango hayo yasingetundikwa ukutani kama ilivyofanyika.

Kazi hiyo ilifanywa na shule ya South Mountain Elementary katika eneo la South Orange.

Mojawapo ya bango liliwaonyesha watumwa kukiwa na mchoro wa msichana wa miaka 12 aliyejulikana kama Anne ambaye aliuzwa kuwa yaya.

Wazazi waliokasirika waliandika katika mtandao wa facebook: Haiingii akilini ni vipi mradi kama huu unaweza kufanywa kuwa funzo la kuwaelimisha wanafunzi kuhusu historia ya Marekani.

Lakini mtu mmoja anayewaangalia wanafunzi, Andrea Espinoza aliambia chombo cha habari cha ABC 7: Ni swala la kihistoria .ilifanyika.Nadhani ni vyema kwa wao kujua.