Rais wa Uturuki alitusi baraza la mawaziri la Uholanzi

Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki asema baraza la mawaziri la Uholanzi lina mabaki ya Ki Nazi
Image caption Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki asema baraza la mawaziri la Uholanzi lina mabaki ya Ki Nazi

Rais Erdogan wa Uturuki amelituhumu baraza la mawaziri la Uholanzi, kwamba limekaa kama mabaki ya Ki-Nazi na kama mafashisti, baada ya baraza hilo kumkatalia waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Uturuki, kutua mjini Rotterdam, kuwashawishi wapigaji kura wa Uturuki waunge mkono kura ya maoni kuhusu katiba ya Uturuki.

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Uholanzi, imesema, juhudi za kutafuta suluhu inayokubalika zilishindikana, pale Uturuki ilipotishia kujibu kwa vikwazo, iwapo ziara ya waziri huyo itakataliwa.

Hapo awali, Rais Erdogan alitumia tusi hilo, kufananisha hatua ya serikali ya Ujerumani kuwa ya ki-Nazi, kwa sababu hizo hizo.

Mvutano umezidi Uholanzi, kwa sababu ya uchaguzi wa wabunge wa juma lijalo, pamoja na kura ya maoni kuhusu katiba ya Uturuki, mwezi ujao.

Mabadiliko hayo ya katiba yatazidisha madaraka ya Rais Erdogan.