Bashar al-Assad: Syria kushirikiana na Marekani

Rais Bashar al-Assad wa Syria
Image caption Rais Bashar al-Assad wa Syria

Rais Bashar al-Assad wa Syria ameelezea ahadi ya Rais Trump, kulishinda kundi la Islamic State, kwamba inatia moyo.

Akizungumza kwenye televisheni, Rais Assad alisema, kimsingi, kuna uwezekano wa kushirikiana, baina ya serikali yake na serikali mpya ya Marekani.

Lakini alisema, kitu kama hicho hakikupata kutokea kabla, na alielezea kuwepo kwa wanajeshi wa Marekani kaskazini mwa Syria, kwamba ni uvamizi.

Wakati wote wa vita vya miaka 6, Marekani imekuwa upande wa makundi yanayoipinga serikali ya Rais Assad.