Gabon: Serikali kuzungumza na upinzani mwisho wa mwezi

Rais Omar Bongo wa Gabon
Image caption Rais Omar Bongo wa Gabon

Serikali ya Gabon imetangaza kwamba mazungumzo na upande wa upinzani yataanza mwisho wa mwezi, lakini kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Jean Ping, amesema hatoshiriki.

Rais wa Gabon, Ali Bongo, alipendekeza mazungumzo hayo, baada ya yeye kutangazwa alishinda katika uchaguzi wa mwaka jana, uliokuwa na utata.

Bwana Ping anasema kulifanywa udanganyifu katika uchaguzi, na angelifaa yeye kuapishwa kama rais, badala ya Bwana Bongo.

Familia ya Bwana Bongo imeongoza Gabon kwa nusu karne.

Upinzani unasema watu kadha walikufa katika ghasia zilizofuatia uchaguzi.