Buhari: Sijawahi kuwa mgonjwa kupitia kiasi

Rais Buhari aliwasili kutoka Uingereza kwa ziara rasmi ya kimatibabu
Image caption Rais Buhari aliwasili kutoka Uingereza kwa ziara rasmi ya kimatibabu

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa hajawahi kuwa mgonjwa kupita kiasi kama alivyokuwa katika majuma ya hivi karibuni.

Alikuwa akizungumza na maafisa wakuu mjini Abuja baada ya kurudi nyumba kufuatia likizo ya wiki saba ya kimatibabu nchini Uingereza.

Kutokuwepo kwake kulizua wasiwasi nchini Nigeria huku watu wakitoa uvumi kuhusu afya yake.

Makamu wa rais Yemi Osinbajo alichuku majukumu ya rais na msemaji wa rais amesema kuwa iongozi huyo atachukua mamlaka kuanzia siku ya Jumatatu.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 74 aliwasili katika uwanja wa Kaduna kutoka Uingereza siku ya Ijumaa alfajiri.

Licha ya kuzungumza kuhusu alivyokuwa akijihisi, bwana Buhari hakutoa maelezo yoyote kuhusu hali yake.