Muimbaji Joni Sledge, afariki

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joni kiimba katika bendi ya Sister Sledge ambayo inajulikana kwa kibao 'We Are Family'

Muimbaji, Joni Sledge, ambaye alisaidia pakubwa kuboresha magoma ya densi miaka ya sabini, amefariki nyumbani kwake huko Phoenix, katika jimbo la Arizona nchini Marekani.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 60.

Kilichosababisha kifo chake bado hakijabainika.

Wakiwa pamoja na dada zake watatu, Joni Sledge aliunda bendi mwaka 1971-- lakini hadi mwaka 1979 ndipo walipopata ufanisi mkubwa walipochomoa kibao "We are Family" -- wimbo ambao unaonekana na wengi kama wa kuleta umoja na kuwapa nguvu kina dada.

Image caption Sister Sledge wakiigiza jukwaani

Mbali na kuteuliwa katika tuzo ya Grammy- ngoma "We Are Family", kibao ambacho kiliuza zaidi ya santuri milioni moja tangu kilipozinduliwa mnamo mwaka 1978, pia kundi hilo lilifahamika kwa densi, Lost in the Music.

Mwaka 2015 walimuimbia Papa Francis wa Vatican kibao "We Are Family for Pope Francis"