Wasichana 2 washambuliaji wa kujitolea mhanga wauawa Nigeria

Boko Haram Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram

Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa wasichana wawili wanaokisiwa kuwa washambuliaji wa kujitoa mhanga, wameuawa kwa kupigwa risasi wakati walijaribu kuingia kaskazini mashariki mwa mji wa Maiduguri saa za usiku.

Polisi walisema kuwa kikosi cha kupambana na wanamgambo wa jihad kiliwafyatulia risasi wasichana hao wenye umri wa miaka 18 kabla ya kulipua milipuko yao.

Milipuko hiyo kisha iliharibiwa kwa nji salama.

Kundi la Boko Haram ambalo lilianzia mjini Maiduguri, limekuwa likiwatumia wanawake kama washambuliaji wa kujitoa mhanga.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la Boko Haram limekuwa likiwatumia wanawake kama washambuliaji wa kujitoa mhanga.