Gari laua watu 34 Haiti

mji wa Gonaives upo kilomita 150 kutoka Kaskazini mwa mji mkuu Port-au-Prince.
Image caption mji wa Gonaives upo kilomita 150 kutoka Kaskazini mwa mji mkuu Port-au-Prince.

Gari moja nchini Haiti limevamia katikati ya umati wa watu na kuuwa 34 na kuwajeruhi wengine 15.

Tukio hilo limetokea katika mji wa Gonaives Kaskazini mwa mji mkuu wa Port au Prince.

Maofisa wanasema gari hilo awali liliingia njia ya watembea kwa miguu na kumuua mtu mmoja.

Baada ya hapo dereva wa gari hilo aliongeza mwendo na kuvamia kundi la watu hao.

Maafisa wameanzisha uchunguzi wa sababu halisi ya ajali hiyo.