Belarus: viongozi wa upinzani wakamatwa kwa maandamano

Wengi wa waandamanaji wanasema kodi hiyo ni batili
Image caption Wengi wa waandamanaji wanasema kodi hiyo ni batili

Mashirika ya kutetea haki za kibinaadam nchini Belarus yamesema baadhi ya viongozi wa upinzani pamoja na waandishi wa habari wamekamatwa wakati wa maandamano ya kupinga kodi kwa watu ambao hawana ajira rasmi.

Mamia ya waandamanaji katika baadhi ya miji wanataka kujiuzulu kwa Rais Alexander Lukashenko ambaye amekaa madarakani kwa robo karne.

Mmoja wa waandamanaji amesema hajawahi kuona raia wa nchi hiyo wakiwa na hasira kama ilivyo hivi sasa.

Image caption Alexander Lukashenko anatajwa na baadhi ya viongozi wa Magharibi kama dikteta wa sasa Ulaya

Lukashenko anasema kodi hiyo ni kwa ajili ya kufuata sheria na maadili na sio kwa ajili ya kuongeza mapato kama wengi wanavyodhani.