Vita vyakwamisha misaada ya kibinaadam Sudan Kusini

Inasemekana kuwa katika eneo la milima ya Nuba kuna njaa iliyotopea
Maelezo ya picha,

Inasemekana kuwa katika eneo la milima ya Nuba kuna njaa iliyotopea

Shirika moja la kutoa misaada ya kibinaadam nchini Sudan Kusini limesema kuwa ni muhimu kutafutwa Kwa suluhisho la haraka ili kuweza kupelekwa misaada ya kibinaadam katika sehemu zinazoshikiliwa na waasi kwenye milima ya Nuba.

Inasemekana kuwa katika eneo hilo kuna njaa iliyotopea.

Shirika hilo linasema kuwa kuna uhaba mkubwa wa chakula katika sehemu nyingi zinazozunguka mlima wa Nuba.

Serikali ya Sudan Kusini tiyari imekubali kupelekwa misaada katika eneo hilo, huku ugumu ukibaki kwa waasi waliopo eneo hilo ambao mpaka sasa bado hawajakubali.