Mji wa Paris kukabiliana na ongezeko la panya

Mji wa Paris kupambana na ongezeko la panya Haki miliki ya picha disney
Image caption Mji wa Paris kupambana na ongezeko la panya

Meya wa mji mkuu wa Ufaransa Paris, Anne Hidalgo ametangaza mipango mipya ya kuweza kudhibiti ongezeko la panya na kusafisha pia vichungio vya sigara vilivyozagaa mitaani.

Akihojiwa na Jarida moja la kila wiki nchini humo, meya huyo Anne Hidalgo amesema mji huo utatumia kiasi cha dola za Marekani milioni 1.6 kununua mitego mipya kwa ajili ya kunasia panya na kuongeza visahani vya kuwekea majivu ya sigara kwenye maeneo ya umma.

Wingi wa panya hao imekuwa ikikadiriwa kuwa kila mkazi mmoja anaweza kumiliki panya wawili.

Desemba mwaka jana, utawala wa mji huo ulifunga baadhi ya bustani za kupumzikia kama sehemu ya kupambana na panya hao.

Meya wa mji wa Paris amewataka pia wamiliki wa migahawa na majengo kuweka zaidi visahani vya kuwekea majivu kwa wavuta sigara katika njia za kuingilia na kutokea.

Wafanyakazi wa manispaa katika mji huo wa Paris wamekuwa wakikusanya tani mia moja na hamsini za vichungi vya sigara kila mwaka.