Shambulizi la bomu laua watu 10 Mogadishu

Juhudi za uokoaji kwa sasa zinaendelea Haki miliki ya picha AP
Image caption Juhudi za uokoaji kwa sasa zinaendelea

Polisi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu, wanasema kuwa bomu la kutegwa ndani ya gari limelipuka kwenye mtaa mmoja wenye shughuli nyingi karibu na mgahawa mmoja.

Takriban watu 10 waliuawa kwenye shambulizi hilo na wengine kadha kujeruhiwa, kwa mujibu wa mtandao wa Radio Shabele nchini humo.

Hakuna kundi lililodai kutekeleza shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la al-Shabab, limekuwa likilenga migahawa mjini Mogadishu.

Huo ndio mlipuko wa pili kuripotiwa hii leo.

Mapema polisi walilifyatulia gari moja risasi wakati lilikata kusimama kwenye kituo cha ukaguzi ndipo gari hilo likalipuka na kumuua dereva.

Mamia ya wanajeshi wa Somalia nao walianda,ana mwishoni mwa wiki kutokana na kutolipwa mishahara ambapo walifunga barabara na kulazimisha biashara kufungwa.