Watoto wa Syria walitaabika zaidi mwaka 2016 kutokana vita

Watoto wa Syria walitaabika zaidi mwaka 2016 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watoto wa Syria walitaabika zaidi mwaka 2016

Watoto nchini Syria walitaabika zaidi mwaka 2016 huku wengi wakiuawa kuliko mwaka wowote ule wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef.

Takriban watoto 652 waliuawa, 255 kati yao karibu na shule mwaka uliopita, ambalo ni ongezeko la asilimia 20 zaidi kutoka kwa idadi ya wale waliouawa mwaka 2015.

Idadi hiyo inajumuisha vifo vilivyotangazwa ikimaanisha kuwa huenda ikawa ni ya juu zaidi.

Unicef inaamini kuwa zaidi ya watoto 850 waliajiriwa kupigana vita mwaka 2016.

Idaia hiyo ni mara dufu ya ile ya mwaka 2015. Wale walioajiriwa walitumwa mstari wa mbele vitani au kutumiwa kama wauaji, washambuliaji wa kujitoa mhanga na walizinzi wa magereza.

Miaka sita iliyopita, maandamano ya kwanza kumpinga Rais Bashar al-Assad yalianza nchini Syria. Maandamano hayo yalisababisha makabiliano makali na kisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watoto wa Syria walitaabika zaidi mwaka 2016

Maandamano ya kwanza yalifanyika kushinikiza kuachiliwa kwa wanafunzi waliokuwa wamekamatwa na kisha kuteswa kwa kuchora michoro ya kuipinga serikali.

Tangu wakati huo idadi ya vifo vya wanafunzi imeongezeka.

Wiki iliyopita shirika la Save the Children lilionya kuwa mamilioni ya watoto nchini Syria huenda wakaishi katika hali msomgo wa mawazo na kusema kuwa huenda hali hiyo ikawa mbaya zaidi ikiwa msaada wa dharura hutatolewa.

Pia lilisema kuwa theluthi mbili ya watoto huenda wamewapotezz wapendwa wao, nyumba yao imebomolewa au kujeruhiwa kwa sababu ya vita.

Haki miliki ya picha Unicef
Image caption Watoto wa Syria walitaabika zaidi mwaka 2016