Mchoro wa Hitler kuwekwa kwenye maonyesho kwa mara ya kwanza

Mchoro wa Hitler kuwekwa kwenye moanyesho kwa mara ya kwanza Haki miliki ya picha Museo della Follia
Image caption Mchoro wa Hitler kuwekwa kwenye moanyesho kwa mara ya kwanza

Mchoro wa Adolf Hitler unatarajiwa kuweka kwa maonyesho kwa mara ya kwanza kwenye makavazi kaskazini mwa Italia.

Mchoro huo mdogo ulikuwa umekodiwa kwa makavazi ya Kijerumani huko Salo, "maarufu kama makavazi ya mawazimu"

Mchoro huo unoonyesha wanaume wawili kwenye meza huku njia ya giza ikionekana nyuma yao.

Licha ya kutajwa kuwa msanii asiye na mwelekeo, kazi yake imepata pesa nyingi kwenye mauzo miaka ya hivi karibuni

Kando na michoro ya Hitler itakuwepo pia ya wasanii mashuhuri wakiwemo Francisco Goya na Francis Bacon.

Maonyesho hayo yatafunguliwa siku ya Jumamosi.

Haki miliki ya picha Hulton Archive
Image caption Adolf Hitler