Scotland kuomba kura ya pili ya uhuru

Kiongozi wa serikali ya Scotland Nicola Sturgeo
Image caption Kiongozi wa serikali ya Scotland Nicola Sturgeo

Kiongozi wa serikali ya Scotland Nicola Sturgeon, amethibitisha kuwa ataomba ruhusa ya kufanywa kura ya maoni ya pili kuhusu uhuru wa Scotland.

Bi Sturgeon anasema kuwa anataka kura kufanyika kati ya mwaka 2018 na 2019.

Kiongozi huyo anasema hatua hiyo inahitajika ili kulinda maslahi ya Scotland baada ya Uingereza kupiga kura ya kuondoka EU.

Anasema ataliomba bunge la Scotland wiki ijayo kuomba amri kutoka kwa bunge la Uingereza.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wapiga kura wa Scotland walikataa uhuru kwa asilimia 55 kwa 45

Amri hiyo itahitajika kuruhusu kuwepo kwa kura ya maoni kuhusu uhuru .

Waziri mkuu Theresa May hajatamka lolote ikiwa ataruhusu kura hiyo ifanyike.

Msemaji wake alijibu matamshi ya Bi Sturgeon, akisema kuwa ushahidi ulionyesha wazi kuwa watu wengi hawataki ifanyike kura ya maoni ya pili.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicola Sturgeon na Theresa May