Watu milioni 14 kupoteza bima ya afya Marekani

Bima ya Obama Care ilinzishwa March 23, 2010
Image caption Bima ya Obama Care ilinzishwa March 23, 2010

Taasisi moja ya utafiti nchini Marekani imesema kuwa takriban watu milioni 14 watapoteza bima za afya mwaka ujao kama chama cha Republican kitapisha azimio la kuondoa bima ya afya iitwayo Obamacare.

Ofisi ya bajeti ya bunge la Congress imesema kuwa chini ya mfumo mpya, idadi itaongezeka na kufikia milioni 24.

Rais Trump ameunga mkono pendekezo hilo na kusema kuwa, ambalo chama cha Republican kinasema litapunguza gharama.