Angela Merkel aahirisha mkutano wake na Trump Marekani

Josephine Shaw Lowell Memorial Fountain Bryant Park, New York City, 13 March 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kuna baridi kali katika jiji la New York

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahirisha safari yake ya kwenda Washington kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump kutokana na hali mbaya ya hewa.

Maeneo ya kaskazini mashariki mwa Marekani yanakabiliwa na kimbunga kikali.

Katika majimbo ya New York na New Jersey tayari yametangaza hali ya hatari huku upepo mkali wa majira ya baridi, ambao umeambatana na theluji ukiendelea kuvuma maeneo hayo.

Shule zimefungwa na safari za maelfu ya ndege kuahirishwa.

Kimbunga hicho kimepewa jina Stella na kinavuma kwa kasi ya hadi kilomita 100 kwa saa (maili 60 kwa saa).

Kuna uwezekano wa kimbunga hicho kutatiza wasafiri maeneo ya kaskazini mashariki mwa Marekani mapema Jumatano asubuhi, watabiri wa hali ya hewa wanasema.

Wakati mmoja, theluji ilikuwa ikimwagika kwa kasi ya hadi inchi 1-3 (sentimeta 2.5-7.6) kwa saa, kwa mujibu wa Alan Dunham mtaalamu wa hali ya hewa anayehudumu Taunton, Massachusetts.

Haki miliki ya picha Getty Images

Safari hiyo ya Merkel ambayo awali ilipangiwa kufanyika Jumanne sasa imepangiwa kufanyika Ijumaa.

Upepo huo pia umemlazimu waziri mkuu wa eneo la Taoiseach la Ireland Enda Kenny kusitisha ziara yake fupi kwenda Boston na badala yake akatumia treni hadi Washington.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Matrekta yamewekwa tayari kuondoa theluji barabarani Brooklyn, New York

More than 6,500 flights have been cancelled, tracking service

Shirika la FlightAware limesema safari za ndege 6,500 zimeahirishwa New York, Washington, Boston, Baltimore na Philadelphia .

Shule zilifungwa Jumanne katika maeneo ya New York, Providence, Rhode Island na miji mingine kadha Massachusetts na Connecticut.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wasafiri New Jersey wametahadharishwa kuhusu hali mbaya ya hewa

Gavana wa New Jersey Chris Christie pia ametangaza hali ya hatari na kuwataka watumishi wa umma ambao hawahusiki katika shughuli za dharura kusalia manyumbani.

Upepo mkali wa baridi kawaida hufuata kipindi cha joto la kadiri kaskazini mashariki mwa Marekani, lakini Februari iliyopita ulitajwa kuwa mwezi wenye kiwango cha juu zaidi cha joto tangu 1895 maeneo hayo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii