Nywele za kisasa zinavyowavutia wanawake Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Nywele za kisasa zinavyowavutia wanawake na wasichana Kenya

Mtindo wa kutengeneza nywele za asili kwa kuweka matuta umejizolea umaarufu na kuvutia wanawake wengi nchini Kenya ambao huwa wanaamini kwamba wanaonekana ni warembo zaidi wawapo katika mtindo huo.

Hata hivyo, huwa wanahitaji fedha zaidi kujipatia nywele hizo pamoja na bidhaa za kutunza nywele za kisasa ambazo mara nyingi huagizwa kutoka nje ya nchi.

Umaarufu huu umesababisha kuibuka kwa wajasiriamali wanaoagiza bidhaa hizi kutoka nje, na wengine kuviundia nchini Kenya.

Mwandishi wa BBC Paula Odek alihudhuria maonesho ya nywele na mitindo viungani mwa jiji la Nairobi na kuandaa taarifa hii.

Mada zinazohusiana