Baraza la wasichana lenye wanaume pekee laanzishwa Saudia

Baraza la wasichana lisilo na wasichana laanzishwa nchini saudia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Baraza la wasichana lisilo na wasichana laanzishwa nchini saudia

Ni hatua nzuri kwa taifa linalojulikana kwa kutowapatia nafasi wanawake katika maisha ya umma.

Lakini wakati Saudia ilipotaka kuonyesha baraza lake la wasichana katika mkoa wa al-Qassim waliwaapuzilia mbali wanawake.

Picha zilizotolewa kuadhimisha baraza la kwanza la wasichana mkoani Qassim zilionyesha wanaume 13 jukwaani na hakukuwepo hata mwanamke mmoja.

Wanawake walikuwemo katika chumba chengine kupitia video.

Picha hizo za wanaume zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii baada ya mkutano huo kufanyika siku ya Jumamosi.

Imefananishwa na picha nyengine ya rais Donald Trump aliyezungukwa na wanaume akitia saini sera ya uavyaji mimba mnamo mwezi Januari.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha ya baraza hilo ni sawa na ile ya Trump alipotia saini sera ya uavyaji mimba

Uzinduzi huo wa Saudia uliongozwa na mwanamfalme Faisal bin Mishal bin Saud, gavana wa mkoa huo aliyesema kuwa anafurahia mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika katika ufalme huo.

''Katika mkoa wa Qassim tunawaangalia wanawake, akina dada zetu na wanaume na tunahisi tunajukumu kubwa la kuwafungulia fursa zitakazowahudumia wanawake na wasichana'', ,alisema.

Baraza hilo la wasichana liko chini ya uenyenkiti wa mwanamfalme Abir Bint Salman, na mkewe ambaye hakuwepo katika picha hiyo.