Wakimbizi wapewa fedha Magharibi Tanzania

Shirika la mpango wa chakula Duniani WFP limeanza kutoa kiasi cha shilingi elfu 20 pesa taslimu za Kitanzania, sawa na dola tisa, kwa wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania, ambapo zaidi ya wakimbizi laki moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi wamehifadhiwa katika kambi hiyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa wakimbizi kupewa msaada wa chakula kwa mfumo wa kupokea fedha tangu kuwepo kwa kambi za wakimbizi nchini Tanzania.

Leonard Mubali alifika katika kambi na kutuandalia taarifa ifuatayo.