Jinsi nilivyowapelekea wahalifu simu gerezani

James Almond
Image caption James Almond

Ndege zisizokuwa na rubani au drones, zimekuwa maarufu kwa kutumiwa kupeleka madawa ya kulevya na simu za mkononi ndani ya magereza, lakini hata hivyo wafanyakazi wa magereza kuwapelekea wafungwa simu pia ni njia nyingine maarufu.

Gumzo na mfungwa mmoja kuhusu kandanda lilisababisha James Almond kuvunja sheria mwenyewe.

Akiwa mfanyakazi wa gereza wakati huo, alikuwa akifanya mazungumzo na mfungwa kuhusu klabu yake anayopenda ya Manchester United, wakati mfungwa aliyekuwa akizungumza naye alimuomba ampelekee simu ambayo ni marufuku ndani ya gereza.

"Alikuwa akiniuliza kila siku," Almond alisema.

Huo ulikuwa mwaka 2014 wakati alikuwa ameajiriwa katika gereza moja eneo la Rutland.

Almond mwenye umri wa miaka 33 kisha akakubali kupeleka simu na kafanya hivyo kwa wiki kadha kabla ya kupatwa na kusababisha yenye mwenye kufungwa.

Sasa anasimulia hadithi yake ili wengine wapate kuelewa shinikizo alililokumbana nalo kutoka kwa mfungwa.

Kesi yake inaangazia tatizo la ufisadi miongoni mwa wafanyakazi wa magereza nchini Uingereza na Wales.

Image caption Simu za mkononi ni kitu cha thamani kwa sababu huwawezesha wafungwa kuwasiliana na familia na wahalifu wengine

James Almond hakutarajia hilo wakati akianza kufanya kazi katika gereza hilo lililo na wafungwa 670 wa kiume, wengi wanaotumikia vifungo vya makosa ya ghasia.

"Nahisi nilijipata kimakoaa katika hali hiyo kwa sababu nilikuwa na msongo wa mawazo baada ya kifo cha babangu.

"Na hili ndilo wafungwa hugundua kwa haraka sana," anasema Almond.

Uingizaji wa bahasha

Mfungwa Almond alifanya mazungumzo naye, kisha akaanza kumtisha kuwa angeidhuru familia yake ikiwa hangeitikia kupeleka simu.

Alinitisha sana hasa wakati alisema kuwa aliwafahamu wapwa wangu.

Jamaa huyo alikuwa gerezani kwa wizi wa kutumia nguvu na sikujua kile alikuwa na uwezo wa kufanya.

Vitisha hivyo vilisababisha Almond kukubali kupeleka simu kwa wafungwa.

Simu za mkononi ni kitu cha thamani kwa sababu huwawezesha wafungwa kuwasiliana na familia na wahalifu wengine walio nje.

Almond alitekeleza hilo kwa kuchukua bahasha kutoka kwa mtu ambaye hakumfahamu na kuiweka kwa mfuko wake na kisha kupita nayo kwenye milango ya gereza bila kutambuliwa.

"Ilikuwa ni hatua hatari sana hadi siku moja waliamua kuwakagua wafanyakazi wa gereza," anasema hakukaguliwa kwa kipindi cha miezi sita alifanya kazi.

Anasema alilipwa pauni 500 kwa kila bahasha, na alifanya hivyo mara mbili kwa wiki.

John Podmore, ambaye amefanya kazi katika idara ya magereza kwa miaka 25 anaamini kuwa mshahara kidogo na kutokuwepo mafunzo mema ni baadhi ya masuala yanayochangia wafanyakazi kuingiza bidhaa gerezani.