Mgombea urais nchini Ufaransa kuchunguzwa

Francois Fillon Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Francois Fillon

Mgombea kiti cha urais nchini Ufaransa Francois Fillon, sasa anachunguzwa rasmi kwa tuhuma kwamba alimfanyia mipango mkewe muingereza, alipwe mshahara kwa kazi ya usaidzi katika bunge.

Fillon anakana madai hayo na kudai ataendelea na kampeni za uchaguzi huo wa mwezi ujao.

Bwana Fillon anadaiwa kumlipa mkewe na wanawe wawili kazi iliyokuw ifanywe bungeni lakini haikufanywa madai ambayo wote wanakanusha.

Wakati mmoja Fillon alisema kwamba atajiuzulu kama mgombea wa chama cha Republican iwapo atachunguzwa rasmi lakini baadaye alibadili msimamo huo.

Anasema kuwa atakabiliana na kile anachokitaja kuwa vita vya kisiasa.

Hadi hivi majuzi alionekana kama mgombea bora kwenye uchaguzi ambao utaandaliwa Aprili na Mei.

Lakini waziri huyo mkuu wa zamani anaonekana kuteleza na kujipata nyuma ya mgombea wa chama cha National Front, Marine Le Pe na Emmanuel Macron.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marine Le Pen anajitaja kuwa mgombea bora wa urais Ufaransa