Uzalishaji wa zao la coca waongezeka maradufu nchini Colombia

Moja ya shamba kubwa lililogundulika na serikali hivi karibuni
Image caption Moja ya shamba kubwa lililogundulika na serikali hivi karibuni

Serikali ya Marekani imesema uzalishaji wa zao la coca inayotengeneza cocaine umevuka mipaka nchini Colombia.

Ripoti zinasema kuwa maeneo ya uzalishaji yameongezeka mara mbili ya ilivyokuwa miaka mitano iliyopita ikiwa ni takriban hekta laki moja na elfu tisini.

Hii inaweza kutengeneza mpaka kilo mia saba za cocaine kwa mwaka.

Image caption Kipindi cha nyuma baadhi ya mashamba haya yalimilikiwa na waasi lakini sasa wanashirikiana na serikali katika kuyateteketeza

Serikali ya Marekani inaamini kuwa kuachwa kupuliziwa kwa dawa maalumu ya kukausha zao hilo kwa njia ya helikopta imekuwa sababu ya kuongezeka kwake.

Serikali ya Colombia imesema hekta elfu hamsini zitateketezwa mwaka huu na zilizobaki zitateketezwa taratibu.