Siku ya Wanaume huadhimishwa lini?

Siku ya wanaume Haki miliki ya picha Thinkstock

Mwezi Machi kila mwaka, wanaume katika mitandao ya kijamii hulalamika wanawake wanapokuwa wanaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kila tarehe 8 Machi.

Huwa wanalalamika kwamba ni wanawake pekee wanaoonekana kuangaziwa kimataifa na kwamba hakuna anayewajali wanaume.

Katika hili, huwa wamekosea pahali kwani ipo Siku ya Kimataifa ya Wanaume, na imekuwepo kwa miaka mingi.

Siku yenyewe ni 19 Novemba.

Mchekeshaji Richard Herring mwaka uliopita, alikerwa sana na wanaume waliokuwa wakilalamika kwamba hakuna siku ya wanaume, na alifika kwenye Twitter kuwafahamisha.

Siku ya Kimataifa ya Wanaume imekuwa ikiadhimishwa tangu mwaka 1999 na hutumiwa kuhamasisha watu na kuangazia masuala yanayowatatiza wanaume, yakiwemo matatizo ya afya ya kiakili na changamoto katika maisha ya familia.

Wanawake wengi wa umri wa chini ya miaka 45 hufariki kwa kujiua kuliko njia nyingine zote, suala linalotilia mkazo hitaji la kuangazia hali ya kiakili ya wanaume.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii