Rais wa Korea Kusini awatelekeza mbwa wake ikulu

Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".
Maelezo ya picha,

Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".

Makundi ya kutetea haki za wanyama yamemlaumu rais wa Korea Kusini aliyeondoka madarakani Park Geun-hye, kwa kuwatelekeza mbwa wake wakati aliondoka ikulu

Mzozo huo unaibuka wakati Bi Park anaitwa kuhojiwa kufuatia kutajwa kama mshukiwa kwenye sakata kubwa ya ufisadi ambayo ilichangia kuondolewa kwake madarakani.

Alitimuliwa wiki iliyopita wakati mahakama ya katiba ilidumisha uamuzi wa kuondolewa kwake madarakani.

Korea Kusini itafanya uchaguzi wake wa urais tarahe 9 mwezi Mei.

Bi Park ndiye rais wa kwanza aliyechagulia kidemokrasia kuondolewa madarakani.

Maelezo ya picha,

Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".

Mwishoni mwa wiki Bi Park aliondoka ikulu ya rais ambayo inafahamika kam Cheong Wa Dae na kuelekea nyumbani kwake kwenye mtaa wa kifahari mjini Seoul.

Mbwa wake tisa hawakuwa miongoni kwa vitu alivyoandamana navyo.

Kundi la kupinga unyanyasaji wa wanyama linasema kuwa alikiuka haki za wanyama kwa kuwaacha nyuma.

Msemaji wa ikulu alikana madai kuwa Bi Park aliwatelekeza mbwa wake na kuliambia shirika la Reuters kuwa mbwa hao waliachwa nyuma kwa sababu haingekuwa vyema wao kuondolewa kwenye makazi yao.

"Aliwaambia wafanyakazi wa ikulu kuwa wawatunze mbwa hao na wawatafutia makao ikiwa itawezekana," msemaji wake alisema,

Maelezo ya picha,

Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".

Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".

Korea Kusini imekuwa ikiongozwa na waziri mkuu Hwang Kyo-ahn tangu bunge lipige kura ya kumuondoa madarakani mwezi Disemba.

Tarehe ya uchaguzi wa rais ilitangazwa wakati wa mkutano wa mawaziri siku ya Jumatano

Wakati wa mkutano huo bwana Hwang alisema kuwa hatawania urais, hatua ambayo ilikuwa pigo kwa chama cha Conservative.