Watu 2 watekwa na shule kuchomwa Burkina Fasso

Ramani ya Burkina Fasso
Image caption Ramani ya Burkina Fasso

Watu wawili wametekwa nyara huku shule ikichomwa katika shambulio lililotekelezwa Kaskazini mwa Burkina Fasso ,ambapo wanajihad hivi majuzi walitishia taasi za elimu .

Shule ya Baraboule iliopo karibu na Djibo mkoani Soum kaskazini mwa Burkina Faso ilichomwa na watu wasiojulikana siku ya Jumanne kulingana na mtandao mmoja wa taifa hilo Burkina24.

Mtandao huo wa kibinafsi ulimnukuu afisa mmoja wa eneo hilo akithibitisha utekaji huo na shambulio katika shule hiyo.

Wanajihad kutoka kundi la Ansar-al-Islam waliwaua watu 3 katika shambulizi la eneo la Kourfayel, katika jimbo hilo hilo tarehe 3 mwezi Machi.

Mwalimu mkuu alikuwa miongoni mwa waathiriwa.

Walimu waliandamana dhidi ya shambulio hilo huku wakitaka usalama kuimarishwa.

Wapiganaji wa Kiislamu waliripoti kuagiza shule katika eneo hilo kufunza kwa lugha ya Kiarabu badala ya lugha ya Kifaransa ambayo ndio lugha rasmi.