Buibui hula zaidi ya tani milioni 400 za wadudu kila mwaka duniani

Bui bui hula zaidi ya tani milioni 400 za wadudu kila mwaka duniani Haki miliki ya picha David E Hill
Image caption Bui bui hula zaidi ya tani milioni 400 za wadudu kila mwaka duniani

Wanasayansi wamefanya hesabu na kugundua kuwa buibui wote walio katika sayari ya dunia, hula kati ya tani 400 na 800 ya wadudu kila mwaka.

Watafiti hao walikuwa wakichunguza umuhimu wa kiuchumi wa buibui.

Wanasema kuwa hamu yao ya kula inamaanisha kuwa wanakula karibu kiwango kimoja cha nyama na samaki ambayo huliwa na binadamu kila mwaka.

Matokeo hayo yamechapishwa katika nakala ya Science of Nature.

Dr Martin Nyffeler kutoka cho cha sayansi cha Basel ambaye aliongoza utafiti huo, alichochewa na kitabu cha mwaka 1958, kinachofahamika kama dunia ya buibui, ambapo mwanasayansi raia wa Uingereza anadai kuwa uzito wa wadudu wanaouawa kila mwaka na buibui nchini Uingerzea, ilizidi uzito wa watu wote nchini humo.

Haki miliki ya picha David E Hill
Image caption Bui bui hula zaidi ya tani milioni 400 za wadudu kila mwaka duniani

Baada ya miongo minne ya kukusanya takwimu, alipata taarifa za kutosha kuweza kubaini ni kiwamgo kipi cha chakula buibui wanakula.

Dr Nyffeler anasema kwa bui bui wote duniani ambao ni wana uzito wa tani milioni 25, wanawinda na kula kati ya tani milioni 400 na 800 za wadudu kila mwaka.

Sasa wanasayansi wanasema kuwa utafiti huo utatoa hamasisho kuhusu umuhimu kwa buibui duniani.

"Buibui huua na kula idadi kubwa ya wadudu waharibifu, na kwa kufanya hivyo hulinda mimea wasiharibiwe," alisema Dr Nyffeler.