Trump ataka kupunguza matumizi ya mafuta kwenye magari

Trump amehakikisha kufanyiwa kazi mapendekezo hayo
Maelezo ya picha,

Trump amehakikisha kufanyiwa kazi mapendekezo hayo

Rais wa Marekani Donald Trump ametaka kuchunguzwa kwa uwezo wa utumiaji mafuta wa vyombo vya moto ambao nchini humo.

Akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza magari cha Michigan, Motor, Trump amesema serikali itakisaidia kiwanda hicho ili magari hayo yatengenezwe tena kwa wingi Marekani.

Kiwanda kicho kimemtaka Trump kuangalia tena sera ya uzingatiaji kiwango cha utumiaji mafuta kwa magari ikiwa ni kilomita 23 kwa lita moja.

Mkuu wa kitengo cha kutunza mazingira Marekani Scott Pruitt amesema viwango vya sasa vinaumiza makamouni mengi na hata wakarekani kwa ujumla.