Mark Rutte: Waholanzi hawataki umaarufu usio na tija

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte
Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amese matokeo ya uchaguzi mkuu nchini mwake yamedhihirisha kuwa waholanzi wamekataa kile kinachoitwa umaarufu usio na maana.

Kwa kura zaidi ya nusu ya zilizopigwa tiyari chama chake cha mrengo wa kulia cha kiliberali kimemshinda kwa urahisi chama cha Geert Wilders kinachopinga uhamiaji na uislamu nchini humo.

Lakini chama hicho kimeshinda viti bungeni kama ilivyo kwa vyama vingine mfano Christian Democrats, GreenLeft party

Maelezo ya picha,

Furaha ilitawala kwa wafuasi wa chama cha Rutte

Muungano wa takriban vyama vinne unahitajika ili kuunda serikali kuu jambo linaloweza kuchukua majuma kadhaa ama hata mwezi mzima.