Trump akumbana na wakati mgumu kupinga uhamiaji

Zuio hilo lilisababisha maandamano nchi nzima
Image caption Zuio hilo lilisababisha maandamano nchi nzima

Majaji nchini Marekani wamempa wakati mgumu Rais Donald Trump baada ya kupinga sheria mpya ya uhamiaji inayowazuia wageni kutoka baadhi ya nchi, nyingi zikiwa za Kiislam kuingia Marekani.

Zuio hilo la majaji limekuja ikiwa ni saa chache kabla ya sheria hiyo kuanza kutumika rasmi.

Hakimu katika jimbo la Hawaii akishirikiana na wanasheria wa serikali wamesema zuio hilo litawanyima haki waislam wa Marekani sambamba na wahamiaji.

Image caption Trump amewaambia wananchi wa Nashville kuwa atapeleka kesi hiyo mahakama za juu

Trump amesema kuwa zuio hilo la makahama ni la kushangaza na sio haki na kupanga kuipeleka kesi hiyo katika mahakama za juu zaidi.