Mji huu jimbo la Oregon Marekani unauzwa $3.8m

Tiller

Mji wote wa Tiller, katika jimbo la Oregon nchini Marekani unauzwa, bei yake ikiwa $3.8m (£3.1m).

Mji huo unapatikana eneo ambalo halina watu wengi ambalo lipo umbali wa kilomita 362 kusini mwa mji wa Portland.

Miongoni mwa vitu vinavyouzwa, kuna nyumba sita, jumba moja lenye vyumba vingi vya makazi, kituo cha petroli na duka moja.

Wakazi takriban 250 huishi maeneo yaliyo karibu na mji huo.

Wakazi walianza kuuhama mji huo baada ya kudorora kwa biashara ya mbao na kufungwa kwa kiwanda cha kupasulia mbao.

Mji wa Tiller ulianza kuuzwa mara ya kwanza mwaka 2015 shule ya msingi ya zamani haikuwa imejumuishwa miongoni mwa vilivyokuwa vinauzwa.

Ni wakazi wawili pekee ambao kwa sasa bado wanaishi katika mji wa Tiller wenyewe. Wakazi hao ni mwalimu wa zamani ambaye anaishi karibu na shule iliyokuwa ikitumiwa zamani, pamoja na mhubiri wa kanisa moja.

Vipande vyao vya ardhi haviuzwi.

Maelezo ya picha,

Mji wa Tiller umezingirwa na milima na msitu

Maelezo ya picha,

Maporomoko ya maji ya South Umpqua yanapatikana karibu na mji wa Tiller

Maelezo ya picha,

Nyumba moja mjini Tiller

Maelezo ya picha,

Duka kuu mjini Tiller bila linauzwa, lakini linauzwa kando

Maelezo ya picha,

Wapenzi wa filamu ya Walking Dead wanaweza kupendezwa na duka hili

Maelezo ya picha,

Shule hii ya msingi ya zamani pia inauzwa, pamoja na paa anayeishi humo

Maelezo ya picha,

Chumba cha kufanyia mazoezi ya viungo shuleni humo

Mbona mtu atake kuishi humo?

"Pesa kutoka kwa serikali kuu za kutumiwa katika biashara ya kupasua mbao zilipoanza kupungua, kiwanda kilifungwa," anasema Garrett Zoller, mmiliki wa shirika la Land and Wildlife.

"Na kiwanda kilipofungwa, wengi wa wapasuaji mbao walianza kuondoka."

Familia inayomiliki mji wa Tiller kwa sasa ilinunua mji huo kipande kwa kipande familia nyingine zilipoendelea kuhama.

Miongoni mwa walioonesha nia ya kutaka kununua mji huo ni wawekezaji kutoka China, pamoja na watu wanaotaka kuanzisha taasisi za matibabu au kukuza miti.