Polisi wa kimataifa wawasaka wauaji wa Kim Jong nam

Polisi wa kimataifa Interpol wametoa ilani uya kukamatwa kwa wauaji wanne wa Kim Jong nam
Image caption Polisi wa kimataifa Interpol wametoa ilani uya kukamatwa kwa wauaji wanne wa Kim Jong nam

Polisi wa kimataifa, Interpol wametoa ilani sawa na waranti ya kimataifa ya kuwakamata raia wanne wa Korea Kaskazini ambao wanatakikana kuhusiana na mauaji ya ndugu wa kambo wa Rais wa Korea Kaskazini.

Idara ya polisi wa Malaysia, inasema kuwa wamepata ilani hiyo baada ya Kim Jong Nam, kuwekewa sumu katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kuala Lumpur.

Ilani hiyo ya Interpol inaorodhesha majina ya watu wanne walio na umri kati ya miaka 30 na 56 na ambao wameondoka Malaysia na wanaaminika kuwa nchini Korea Kaskazini.