Muuguzi achomwa na mgonjwa hadi kufa Israel

Muuguzi wa Israel achomwa na mgonjwa hadi kufa Haki miliki ya picha MDA SPOKESPERSON
Image caption Muuguzi wa Israel achomwa na mgonjwa hadi kufa

Muuguzi mmoja nchini Israel amefariki baada ya kuchomwa akiwa hai na mgonjwa katika eneo la Holon kusini mwa Tel aviv.

Tova Kararo mwenye umri wa miaka 56 alimwagiwa mafuta na kuchomwa baada ya kujibizana na mgonjwa ambaye alikuwa hajaridhika kulingana na afisa mmoja wa polisi.

Mshukiwa huyo ambaye yuko katika umri wa miaka 70 alitoroka eneo la mkasa huo kwa kutumia gari lakini akakamatwa baadaye.

Vyombo vingi vya habari nchini Israel vimeripoti kwamba mshukiwa huyo alikuwa manusura wa holocaust anayeugua ugonjwa wa akili.

Haki miliki ya picha MDA SPOKESPERSON
Image caption Muuguzi huyo alifanyiwa matibabu ya dharura lakini hakupona

Mkuu wa polisi katika eneo hilo Sigal Bar Tzvi alisema kuwa mtu huyo aliwasili katika kituo hicho cha afya na alidaiwa kwamba hakuridhishwa na matibabu aliyopata.

Baada ya kujibizana, alimmwagia muuguzi aliyemtibu na kumchoma, alinukuliwa na mtandao wa habari wa Ynet News akisema.

Harakati za kumfufua ziligonga mwamba na akatangazwa kuaga dunia.