Mhubiri apata almasi ya mamilioni ya dola Sierra Leone

Wachimba migodi wa kujitegemea ni wengi kwenye migodi yenye almasi nyingi nchini Sierra Leone. Haki miliki ya picha Olivia Acland
Image caption Wachimba migodi wa kujitegemea ni wengi kwenye migodi yenye almasi nyingi nchini Sierra Leone.

Mhubiri mmoja wa kikiristo amepata moja ya almasi kubwa zaidi kuwa kupatikana duniani kwenye wilaya ya Kano nchini Sierra Leone.

Almasi hiyo yenye uzito wa karati 709 kwa sasa imefungiwa kwenye benki kuu nchini Sierra Leone mjini Free Town. Ni moja ya almasi 20 kubwa zaidi kuwai kupatikana.

Wachimba migodi wa kujitegemea ni wengi kwenye migodi yenye almasi nyingi nchini Sierra Leone.

Lakini kuna maswali ikiwa jamii itanufaika kutokana na kupatikana kwa almasi hiyo.

Almasi hiyo iliyogunduliwa na Emmanuel Momoh ambayo thamani yake bado haijatangazwa ndiyo ya pili kubwa zaidi kuwai kupatikana nchini Sierra Leone tangu mwaka 1972 wakati almasi nyingi ya karati 969 ilipatikana.

Haki miliki ya picha Umaru Fofana
Image caption Almasi hiyo ina uzito wa karati 709

Kwanza ilipelekwa kwa Rais Ernest Bai Koroma siku ya Jumatano kabla ya kupelekwa benki kuu.

Rais alimshukuru Chifu wa eneo hilo na watu wake kwa kutoisafirisha almasi hiyo nje ya nchi.

Bwana Koroma alisema kuwa wamiliki wa almasi hiyo watapata haki yao na itainufaisha nchi.

Sierra Leone ni maarufu kwa sekta ya almasi.

Biashara ya almasi ilichochoea vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muongo mmoja wakati makundi ya waasi yalifanya biashara ya kubadilishana almasi na silaha