"Vita vya mikate" vyazuka Venezuela

Maduka ambapo watu hupanga milolongo yatachukuliwa hatua
Maelezo ya picha,

Maduka ambapo watu hupanga milolongo yatachukuliwa hatua

Serikali ya Venezuela inasema kuwa itatwaa biashara za kuoka mikate, ikiwa zitashindwa kutimiza masharti ya serikali yenye lengo la kutatua uhaba wa mikate nchini humo.

Kwenye mzozo unaozidi kukua kati ya serikali na wafanyabiashara wa mikate, maafisa walisema kwa wenye biashara ya mikate watapigwa faini ikiwa watu watapanga milologo kununua mikate.

Uhaba mkubwa wa bidhaa muhimu una maanisha kuwa raia nchini Venezuela, mara kadha kadha hupanga milolongo kawa saa kadha kunua bidhaa.

Maelezo ya picha,

Serikali imewalaumu waokaji mikate kwa uhaba huo, ikisema kuwa wao hutumia unga wanaopewa kupika bidhaa tofauti licha ya mikate.

Serikali inasema kuwa uhaba huo umesababishwa na "vita vya kiuchumi".

Venezuela haizalishi ngano na huagiza bidhha hiyo kutoka kwa serikali.

Serikali imewalaumu waokaji mikate kwa uhaba huo, ikisema kuwa wao hutumia unga wanaopewa kupika bidhaa tofauti licha ya mikate.

Maelezo ya picha,

Serikali imewalaumu waokaji mikate kwa uhaba huo, ikisema kuwa wao hutumia unga wanaopewa kupika bidhaa tofauti licha ya mikate.

Siku ya Jumapili rais Nicolas Maduro alitangaza kuwa wakaguzi watatumwa kwenda kwa waokaji mikate 709 kote mjini Caracas, kuhakikisha kuwa wanatekeleza sheria hizo mpya.

Alisema kuwa wale ambao hificha mikate kutoka kwa watu watachukuliwa hatua za kisheria.

Naye makamu wa rais Tareck El Aissami ameonya kuwa makampuni ya mikate ambayo hayatii sheria hizo yatatwaliwa na serikali.

Maelezo ya picha,

Serikali imewalaumu waokaji mikate kwa uhaba huo, ikisema kuwa wao hutumia unga wanaopewa kupika bidhaa tofauti licha ya mikate.

Maelezo ya picha,

Ishara za kuonyesha kutokuwepo kwa mikate ni nyingi mjini Caracas