Ahmad achaguliwa rais mpya wa CAF

Ahmad (kushoto) atachukua mahala pa Issa Hayatou (kulia) baada ya karibu miongo mitatu
Maelezo ya picha,

Ahmad (kushoto) atachukua mahala pa Issa Hayatou (kulia) baada ya karibu miongo mitatu

Rais wa muda mrefu wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF, Issa Hayatou, ameshindwa kwenye uchaguzi.

Sasa rais mpya wa shirikisho hilo la soka ni Ahmad Ahmad, kutoka nchini Madagascar ambaye alipata kura 34.

Hayatou ameongoza shirikisho hilo la CAF kwa muda wa miaka 29.

Matokeo hayo yanamaanisha mabadiliko ya uongozi kwa mara ya kwanza tangu Issa Hayatou kutoka Cameroon achaguliwe 1988.

Ahmad ambaye alionekana kuwa na hisia, anakuwa rais wa saba wa shirikisho hilo la soka barani Afrika Caf katika historia ya bodi ya shirikisho hilo lenye miaka 60.

Ahmed mwenye jina moja aliambia BBC baadaye kwamba ''siwezi kuongea wakati huu''.

''lakini nina kitu kimoja tu, namshkuru mungu, nashukuru kikosi changu''.

''Tulifanya juhudu kali na kushinda. Hiyo ilikuwa hatua ya kwanza ,hatua ya pili ni kuboresha soka ya Afrika. Siku nyengine nilidhani nitashinda-leo sikudhani nitashinda''.

Matokeo hayo yamepokelewa na shangwe katika baraza la Caf huku Ahmed akibebwa katika mabega na wafuasi wake na kumpeleka mbele ya jukwaa baada ya matokeo kutangazwa.

Tofauti ni kwamba Hayatou aliandamana na wasaidizi wake katika jukwaa lakini aliwaambia maripota kwamba mambo sio mabaya.

Ahmad baadaye aliongezea: Unapojaribu kufanya kitu, una maanisha kwamba unaweza kufanya .Iwapo siwezi kufanya nisingegombea.

''Huu ni ushindi mzuri sana.Wakati unapoweka jitihada kwa miaka kadhaa na miezi na kufanikiwa,hicho ni kitu kizuri''.

Ahmad ,ambaye alikuwa rais wa shirikisho la soka nchini Madagascar mwaka 2003, anachukua urais wa Caf katika kipindi cha miaka 4 na ameahidi kulifanya shirikisho hilo kuwa la kisasa mbali na kuweka uwazi.

Kazi yake ya kwanza ,alisema awali siku ya Alhamisi kwamba itakuwa kuzindua sheria mpya za maadili huku akisema kuwa maafisa wa soka wa Afrika watachunguzwa maadili yao.

Kuondoka kwa Hayatou ni mabadiliko makubwa kwa soka ya Afrika na raia huyo wa Cameroon pia atapoteza wadhfa wake katika shirikisho la soka duniani Fifa.

Alikuwa amepingwa mara mbili pekee katika ushindani wa wadhfa huo huku akishinda mara zote kwa kura nyingi.

Mara hii alijipatia kura 20 na hivyobasi kumaliza matumaini ya muhula wake wa nane ambapo uongozi wake ungekuwa umeendelea kwa miongo mitatu kwa jumla.

''Mheshimiwa Issa Hayatou amefanya mengi kwa soka ya Afrika lakini ni wakati wa yeye kuondoka'', alisema George Afriye, makamu wa rais wa shirikisho la soka nchini Ghana.

Rais wa shirikisho la soka nchini Liberia Musa Bility aliongezea: Afrika imefanya uamuzi muhimu kwamba tuko tayari kwa mabadiliko.