Watu 2 wajeruhiwa kwenye shambulizi Ufaransa

Watu kadha wapigwa risasi ufaransa
Image caption Watu kadha wapigwa risasi ufaransa

Watu wawili wamejeruhiwa kufuatia ufyatuaji wa risasi uliotokea mji ulio kusini mwa Ufaransa wa Grasse, kwa kujibu wa taarifa za polisi.

Mtu mmoja alikamatwa lakini mwingine bado yuko mafichoni.

Makomando wa kukabiliana na ugaidi walitumwa eneo hilo.

Serikali ya Ufaransa nayo ilituma onyo la shambulizi la kigaidi kupitia mtandao wake wa simu.

Mji wa Grasse ulio maarufu kwa kutengeneza marashi, uko umbali wa kilomita 44 kutoka mji wa Nice, ambapo lori lilitumiwa kufanya shambulizi mwezi Julai na watu 86 wakauawa.

Ufarasa iko chini ya tahadhari kubwa kufuatia misururu ya mashambulizi mabaya ndani ya kipindi cha miezi 18 iliyopita.