Theresa May: Si wakati wa kura ya uhuru Scotland

Theresa May
Image caption Theresa May

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May anasema kuwa sasa si wakati wa kura ya pili ya maoni ya uhuru wa Scotland.

Hata hivyo hakusema ikiwa atatupilia mbali kufanyika kwa kura hiyo siku za usoni.

Kiongozi wa Scotland Nicola Sturgeon, ametaka kufanyika kwa kura ya maoni mwaka 2018 au 2019.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiongozi wa Scotland Nicola Sturgeon

Lakini Bi May anasema kuwa si vizuri kufaninyika kwa kura ya maoni hadi pale uhusiano wa Uingereza na Muungano wa Ulaya ujulikane wazi.

Scotland ilipiga kura kwa asilimia 55 kwa 45 kusalia Uingereza wakati wa kura ya mwezi Septemba mwaka 2014, lakini Bi Sturgeoan anasema kuwa kura ya maoni inahitajika kuruhusu nchi kuamua njia ya kufuata kufuatia kura ya Uingereza kuondoka Muungano wa Ulaya mwaka uliopita.